Jumapili , 20th Apr , 2014

Serikali ya Tanzania imeuonya umoja wa katiba ya wananchi UKAWA kuwa kama hautarudi bungeni kutafuta muaafaka na kuamua kuzunguka nchi nzima kupotosha wananchi, serikali haitawanyamazia.

Waziri mkuu wa Tanzania, mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda

Waziri mkuu Mizengo Pinda ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana wakati akifunga maonyesho ya maadhimisho ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, maadhimisho yaliyofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja.

Waziri mkuu Pinda amesema badala ya kutafuta suluhu ya mazungumzo kwa yaliyotokea bungeni, ukawa wameamua kutorejea bungeni na kuzunguka nchi nzima, na kwamba iwapo watafanya hivyo, basi wao pia watachukua hatua kama hiyo.