Alhamisi , 23rd Jun , 2016

Serikali imeshauriwa kufanya utafiti wa changamoto zinazoikabili Hospitali ya rufaa ya muhimbili kabla ya kuanza kutoa huduma ya Chakula Kwa Wagonjwa wote hospitalini hapo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sikika, Irenei Kiria.

Akazingungumza na East Africa radio, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sikika, Irenei Kiria amesema kuwa utatifi unaonyesha kuwa watu wengi wanaenda hospitalini hapo si Kwa ajili ya kupeleka chakula pekee bali kuwauguza wagonjwa pamoja na kufuatilia matibabu ya wagonjwa hao ikiwemo kuhakikisha wanapitiwa na daktari.

Kiria amesema kuwa Kuna changamoto nyingi katika utekelezaji wa suala hilo na kuongeza kuwa linaweza kufanikiwa endapo kutakua na uboreshaji wa huduma za Afya lakini pia na kuongeza idadi ya wauguzi wa kusimamia suala hilo.

Aidha ameongeza kuwa serikali pia natakiwa kuhakikisha masuala ya kiutawala yanasimamiwa ipasavyo ikiwemo siku ikitokea wagonjwa hawajapata chakula Kwa wakati au hakijaletwa kabisa lakini pia ni nani wa kuwajibishwa endapo utatokea ubadhilifu.

Sauti ya Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sikika, Irenei Kiria