Jumatano , 9th Nov , 2016

Serikali imeahidi kuendelea kusimamia ahadi ya kuwa na serikali ya viwanda ili kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2020, mchango wa viwanda katika pato la taifa unakuwa mpaka kufikia asilimia 15 kutoka kiwango cha sasa cha asilimia 7.3 kwa mwaka.

Sehemu ya kiwanda cha Global Packaging

 

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhem Meru wakati akiweka jiwe la msingi la kiwanda cha kutengeneza vifungashio cha Global Packaging kilichopo Kibaha mkoa wa Pwani, kiwanda kitakachosaidia uongezaji thamani ya vifungashio vya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa nchini.

Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa NDC Bw. Mlingi Mkucha amesema kiwanda hicho ni matokeo ya NDC katika kubaini wawekezaji wazawa walioona fursa za kiuwekezaji lakini wanahitaji kusaidiwa katika kutimiza malengo yao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kiwanda hicho Bw. Joseph Wasonga amesema wao kama wawekezaji wataendelea kumuunga mkono Rais Magufuli katika mipango yake ya kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda ambapo ameiomba serikali iendelee kusimamia na kuratibu upatikanaji mikopo ya masharti nafuu kwa wawekezaji nchini.