Jumanne , 2nd Dec , 2014

Serikali imeshauriwa kuvifuta vyama vya ushirika vinavyo anzishwa bila utaratibu hapa nchini ili kupunguza ubadhilifu wa fedha za wananchi unaojitokeza mara kwa mara.

Mrajisi Mkuu wa Vyama vya Ushirika nchini Tanzania Dkt. Audax Rutabanzibwa.

Hayo yamesemwa na Mrajisi Mkuu wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Kagera Rwenkiko Nestory katika mkutano mkuu wa saba wa Obumwe Talanta Sacos Wilayani Muleba ambapo amesema vyama hivyo vinatakiwa kufutwa haraka iwezekanavyo na akaongeza kuwa vyama hivyo vimekuwa vikishiriki katika ubadhilifu wa pesa za wananchi na hasa wakulima.

Akiongea katika mkutano huo meneja wa Obumwe Shumbu amesema SACCOS hiyo inalenga zaidi kuwainua wakulima na wafugaji wilayani muleba ili waweze kuondokana na tatizo la umasikini linalo wakabili wananchi hao.

Nao baadhi ya wananchi wameelezea namna wanavyo kabiliana na changamoto mbalimbali za maisha ambapo wamekitaka chama hicho, kushirikiana na taasisi nyingine za fedha ili waweze kupatiwa mikopo ya muda mrefu ambayo inaweza kukidhi mahitaji yao.