Jumanne , 5th Mar , 2019

Serikali imepiga marufuku kusafirisha mizigo, vifurushi na bahasha kwenye magari ya abiria, mpaka kuwe na kibali maalum kutoka Mamlaka ya mawailiano nchini (TCRA)

Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano, Mh Mhandisi Atashasta Nditiye alipokuwa akizungumza na watumishi wa taasisi mbalimbali ambazo ziko chini ya wizara hiyo ikiwemo kampuni ya simu nchini TTCL na shirika la Posta Tanzania, mjini Musoma.

Sambamba na hilo Naibu Waziri Nditiye ameitaka SUMATRA kuendesha oparesheni maalum ya kusimamia agizo hilo, na kudhibiti kabisa vitendo hivyo.

Hata hivyo amewataka watendaji wa taasisi hizo kuziendesha taasisi hizo kwa faida, ikiwa ni pamoja na kutumia vema fedha zinatolewa na serikali kuu kama ruzuku, na kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa watendaji watakaobainika kwenda kinyume na maelekezo hayo.