Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.
Hayo ameyabainisha leo Machi 8, 2020, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, wakati akituma salamu za pongezi za kuwatakia heri wanawake wote katika kuadhimisha siku ya wanawake Kimataifa, inayosherehekewa duniani kote.
"Nawapongeza Wanawake wote kwa kuadhimisha siku hii muhimu, mchango wenu kwa familia,jamii na Taifa hauna mfano, Serikali ninayoiongoza itaendelea kuwathamini,kuwaheshimu na kujenga mazingira bora, yatakayowawezesha kutekeleza majukumu yenu ipasavyo" amesema Dkt Magufuli.

