Jumatano , 18th Jun , 2014

Serikali ya Tanzania imesema kumekuwa na ongezeko kubwa la vijana wanaotumia dawa za kulevya nchini hali inayohitaji nguvu za pamoja katika kukabiliana na hali hiyo ili kuwaepusha vijana na matumizi hayo kwa ustawi wa Taifa.

Waziri wa Uchukuzi nchini Tanzania Dkt Harrison Mwakyembe.

Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Uchukuzi nchini Tanzania, Dkt. Harisson Mwakyembe wakati akifungua mkutano unawakutanisha viongozi mbalimbali wa dini nchini kujadili athari za madawa ya kulevya na namna ya kupambana na uingizwaji wa dawa hizo hapa nchini.

Kwa upande wao viongozi wa Dini, Mwenyekiti wa Baraza la viongozi wa Dini wa kupambana na dawa za kulevya, Alhad Musa Salum, Mkurugenzi wa Taasis ya huduma za Dini ya Kikristu Banza Suleiman pamoja na Mchungaji wa Kanisa la KKKT dayosis ya Mashariki na Pwani, Christosila Petro Eliakarata wanasema ongezeko la vijana katika matumizi ya dawa hizo limechangiwa na Taasisi ya kidini kutoshiriki katika mapambano ya matumizi ya dawa hizo.