Ijumaa , 12th Dec , 2014

Serikali imekubali kuachia maeneo ambayo yalipendekezwa yaingizwe kwenye hifadhi ya taifa ya Ruaha wilayani Mbarali ili kuondokana na mgogoro wa muda mrefu wa ardhi baina ya wakazi wanaozunguka hifadhi hiyo na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa TANAPA..

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu .

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu ametoa tamko hilo wakati akizungumza na wandishi wa habari mkoani Mbeya akisema kuwa maeneo ambayo yamekuwa na mgogoro kwa muda mrefu wilayani Mbarali baina ya wananchi na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa ni mali halali ya wananchi na sasa serikali imeamua kuachana nayo ili kumaliza migogoro hiyo.

Mbunge wa Mbarali, Modestus Dickson Kilufi amesema uamuzi huo wa Waziri Nyalandu umezingatia maslahi ya wananchi na kuwa sasa wananchi wataishi kwa amani wakishirikiana na TANAPA kuwalinda wanyama katika Hifadhi ya Ruaha.

Baadhi ya wananchi ambao wamehudhuria mkutano baina ya waziri na uongozi wa wilaya ya Mbarali wamesema wamefurahishwa na uamuzi huo wa serikali ambao utaleta mageuzi yasiyofutika kwenye maisha yao.