Akizungumza leo Bungeni Mjini Dodoma, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndungulile amesema serikali imeaanda mpango wa kuboresha huduma ya afya kwa wanawake wajawazito wa mwaka 2016 hadi 2020.
Dkt. Ndungulile ameongeza kuwa licha ya juhudi hizo za serikali lakini pia wamepata ufadhili wa beki ya Dunia na nchi ya Canada kwa ajili ya kujenga na kuboresha miundombinu ili kuwezesha kutoa huduma za dharura za uzazi ikiwemo upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni
Imedaiwa kwamba Mkoa wa Mwanza una vifo 305 kwa kila vizazi hai laki moja jambo ambalo serikali imeanza kuchukua hatua ili kudhibiti hali hiyo.
