Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Walemavu, Antony Mavunde
Akizungumza leo mjini Dodoma, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Walemavu, Antony Mavunde amesema lengo la kufanya hivyo ni kuweza kuwatoa vijana kushinda vijiweni bila ya kazi maalumu huku wakilalamikia ukosefu wa ajira.
Mhe. Mavunde amesema kuwa kupitia Baraza la Kuwawezesha Wananchi Kiuchumi,(NEEC), Shirila la Kazi Duniani (ILO), Plan International ambao wanatoa misaada kwa vijana wasomi na wafanyabishara kwa kuwapa mitaji na mafunzo ya kufanya shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato.
Aidha, Naibu Waziri huyo amesema kuwa tayari wakuu wa mikoa wameshaambiwa washirikiane na halmashauri zao kwa kutenga eneo maalumu ya kiuchumi kwa ajili ya vijana ili ya kuwawezesha vijana kupata fursa ya kushiriki katika kuinua uchumi wa nchi yao.
Mhe. Mavunde amesema kuwa vijana wengi wapo tayari kwa ajili ya kujiajiri lakini wanakumbana na changamoto ya mitaji pamoja na ukosefu wa kufanya shughuli hizo hivyo serikali imeamua kuchukua jukumu la kuwawezesha ili kujikwamua kiuchumi.