Jumatano , 14th Mei , 2014

Serikali imetenga Sh. Mil. 500 kwa ajili ya kunyunyiza dawa za kuua mazalia ya mbu kwenye maeneo chepechepe jijini Dar-es-salaam, katika jitihada za kukabiliana na ugonjwa wa Dengue.

Mmoja wa mbu anayedaiwa kusambaza virusi vinavyosababisha homa hatari ya dengue.

Naibu waziri wa afya na usatwi wa jamii, Dk. Kebwe Stephen Kebwe aliyasema hayo wakati akitoa kauli ya serikali bungeni jana kuhusu ugonjwa wa homa ya dengue, baada ya mbunge wa kigamboni (CCM) Dk Ndugulile Faustine, kutaka taarifa ya serikali kuhusu hatua zilizochukua kudhibiti ugonjwa huo.

Dk Kebwe alisema wizara imeandaa mpango wa namna ya kukabiliana na ugonjwa huo na kwamba imeshirikisha sekta mbalimbali ambapo mpaka hivi sasa Sh. Mil. 132 zikiwazimetumika kwa ajili ya ugonjwa huo na kwamba fedha zaidi zitaendelea kutolewa.

Aidha, Dkt Kebwe amewaagiza watendaji wa vitongoji kusimamia usafi kwenye maeneo yao, kama sehemu ya kukabiliana na kusambaa kwa ugonjwa huo ambao umekuwa tishio kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake.