
kwa lengo la kudhibiti mionzi katika bidhaa hizo.
Mh Ole Nasha ameto agizo hilo jijini Arusha alipotembelea Tume hiyo ili kujionea jinsi inavyofanya kazi, ambapo amesema ni muhimu vituo hivyo kuwekwa katika mipaka ili kuhakikisha bidhaa zinazoingia na kutoka nchini zinakuwa na viwango vya mionzi inayokubalika kimataifa.
Ameitaka Tume hiyo kutokuishia katika kutekeleza majukumu ya kudhibiti na kuhamasisha matumizi bora ya mionzi bali inapaswa kuanza kuangalia namna bora ya kuhamasisha matumizi chanya ya nuklia kwa maendeleo ya taifa katika nyanja za Afya, Kilimo, maji na teknolojia.
Naibu Waziri Nasha pia ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa maabara ya kisasa kwa ajili ya upimaji wa ubora wa vifaa mbalimbali vya mionzi ikiwemo vifaa tiba vya Tume hiyo, maabara hiyo inajengwa na fedha za serikali kiasi cha shilingi bilioni mbili.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki, Brigedia Jenerali Fulgence Msafiri, amesema, kutokana na upungufu mkubwa wa watumishi walio na weledi katika Teknolojia ya Nuklia imesababisha Taasisi hiyo kukosa watumishi tangu kuanzishwa kwa vituo vya kudhibiti uingizwaji wa bidhaa katika mipaka ya Rusumo, Mtukula, Kabanga, Kigoma, Tunduma, Kasumulu na Daraja la Mkapa.