Alhamisi , 29th Mei , 2014

Serikali ya Tanzania imesema inaendelea kushawishi na kuzikaribisha taasisi za kimataifa zinazojishughulisha na utoaji wa Bima ili kuvutia zaidi uwekezaji na wawekezaji kuwa na moyo wa kuwekeza nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Naibu waziri wa fedha na uchumi nchini Tanzania, Adam Kigoma Ali Malima.

Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi nchini Tanzania Mhe. Adam Malima ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati aliposhiriki katika mkutano wa mwaka wa majadiliano ya ukuzaji wa Bima wa ATI uliokutanisha zaidi ya nchi thelathini za Afrika.

Mh. Malima amesema wawezekezaji katika makampuni hayo ya Bima watasaidia kuwafanya wananchi kuwa na uhakika wa ulinzi wa mali zao endapo lolote litatokea.