Dkt. Titus Kamani akitembelea mabanda ya maonesho ya kimataifa ya kilimo yanayofanyika katika Jiji la Paris nchini Ufaransa,
Mkurugenzi wa Uzalishaji Mifugo na Masoko katika Wizara hiyo, Anuciate Njombe, amesema uzalishaji wa nyama hapa nchini unatokana na ng'ombe, mbuzi, kuku, kondoo umekuwa ukiongezeka kila mwaka kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita.
Bw. Njombe amesema uzalishaji wa nyama umeongezeka kutoka tani laki 388,294 mwaka 2005 hadi kufikia tani 597,757 kwa mwaka 2014/2015 huku ulaji wa nyama kwa mtu ukiongezeka kutoka tani 11 mwaka 2005 hadi kilo 15 mwaka 2014/2015.
Aidha Bw. Njombe amesema biashara ya nyama nje ya nchi imeongezeka kutoka tani 193.5 kwa mwaka 205 na kufikia tani 1685.80 kwa mwaka huu ambapo katika mika 10 iliyopita mauzo ya nyama yalifikia bilioni 101.954 ziliuzwa nje ya nchi.