Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Serikali kujenga vyuo vitatu vya wenye ulemavu

Alhamisi , 4th Aug , 2022

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof. Joyce Ndalichako amesema kuwa serikali imeanza kutekeleza mpango wa kuwawezesha Watu wenye Ulemavu kwa kujenga vyuo vipya vitatu vya ufundi stadi na kuvifanyia marekebisho vituo vinne

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na waandishi wa habari mjini Kasulu leo Agosti 3, 2022, kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi hiyo kwa Mwaka 2021/22 na Mwelekeo wa Bajeti ya Mwaka 2022/23 mjini Kasulu, Kigoma.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kasulu leo Agosti 3, 2022, kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya ofisi hiyo kwa Mwaka 2021/22 na Mwelekeo wa Bajeti ya Mwaka 2022/23. Waziri Ndalichako alisema kuwa serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan imedhamiria kwa dhati kuleta ustawi wa kiuchumi kwa Watu wenye Ulemavu.

Masuala mengine ambayo bajeti hiyo itatekeleza ni pamoja na. Kufanya kaguzi 4,800 katika maeneo ya kazi pamoja na Kuratibu na kusimamia upangaji wa Kima cha Chini Mshahara katika Sekta Binafsi.

Aidha, alieleza kuwa Ofisi hiyo itaratibu suala la Kupunguzwa kwa kiwango cha uchangiaji kwa waajiri wa Sekta Binafsi kutoka asilimia 0.6 hadi kufikia asilimia 0.5 hivyo kuweka uwiano sawa katika uchangiaji baina ya Sekta Binafsi na Sekta ya Umma.

Ndalichako ametaja vipaumbele vingine kuwa ni; Kuratibu mafunzo ya Ujasiriamali, kwa makundi maalum ya vijana (Mama wadogo, Vijana (WAVIU) katika mikoa 6 pamoja na Kutoa Mikopo kwa vikundi vya vijana vilivyokidhi vigezo kwa mujibu wa Mwongozo wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana. Aidha, kiasi cha Shilingi 1,000,000,000 kimetengwa kupitia ofisi hiyo.

Aliongeza kuwa, Serikali itatoa mafunzo kwa vijana 500 juu ya ujuzi wa uchumi wa blue kupitia ufugaji wa Samaki kwa njia ya vizimba; Uchumi wa Bluu una fursa nyingi hivyo Serikali inalenga kutoa Mafunzo haya ili kuwawezesha Vijana kunufaika na fursa hizo.

“Tutajenga Vituo 5 atamizi kwa vijana wanaopata Mafunzo ya uanagenzi, lengo la Vituo hivyo ni kutoa fursa kwa Vijana, kukuza na kuendeleza Ujuzi wao, aidha, Vituo hivyo vitatoa fursa kwa Vijana Wajasiriamali kuongeza Bidhaa zao thamani ili zifikie kiwango cha kuingia sokoni,” alisema

Katika hatua, nyingine  Ndalichako amewashukuru wadau wa UTATU (Serikali, Vyama vya Wafanyakazi, na Waajiri) kwa kutekeleza kwa Sheria za Kazi nchini. Aidha, amewapongeza watumishi wa yake  kwa utekelezaji mzuri wa majukumu ya Ofisi hiyo kwa bajeti ya Mwaka wa Fedha 2021/2022 na amewataka kuendelea kufanya kazi kwa ari, juhudi, ubunifu na kujituma  na kutanguliza uzalendo mbele.
 

HABARI ZAIDI

Sehemu ya Ardhi iliyoathirika na Mabadiliko ya Tabia Nchi

Hizi hapa sababu za hali ya hewa isiyotarajiwa

Picha za Satelaiti Zikionyesha Mwenendo wa Kimbunga Hidaya

Kimbunga Hidaya chaendelea kutawala eneo la Pwani

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wanahabari na Wadau wengine kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo Mei 03, 2024.

Watendaji serikalini ondoeni ukiritimba - Majaliwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT

Wahitimu JKT watakiwa kulinda miradi ya serikali