Jumapili , 3rd Jul , 2016

Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene amesema serikali katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/2017 inatarajia kujenga vituo vya afya 105 katika maeneo mbalimbali nchini.

Waziri Simbachawene ameyasema hayo katika mahojiano maalumu katika kipindi cha Nipashe kinachorushwa na Radio One Jijini Dar es salaam.

''Tumedhamiria kupambana na tatizo kubwa la upungufu wa vituo vya afya nchini na kwa kuanzia unatarajia kujenga vituo hivyo vya afya , na vigezo vitakavyotumika ni kuangalia umbali wa kata moja na nyingine na uwezekano wa wananchi kushiriki tiba katika kata itakayochaguliwa kujengwa kituo.

Aidha Waziri Simbachawene amesema zoezi la kutenga bajeti kwa ajili ya kujenga vituo vya afya nchini ni zoezi endelevu ambapo kila mwaka wa fedha serikali itatenga fedha ili kuweza kupunguza tatizo la upungufu wa vituo tiba hapa nchini lengo likiwa ni kumuonmdolea adha ya kupata matibabu mwananchi.