
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo leo wakati anazungumza na uongozi wa kiwanda cha A to Z kilichopo mkoani Arusha katika ziara yake ambayo imeingia siku ya pili ya kutembelea viwanda mbalimbali mkoani humo ili kujua changamoto zinazokabili viwanda hivyo na serikali kuzitafutia ufumbuzi.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali imetenga fedha za kutosha zitakazotumika kuviimarisha vyuo vya Veta ili viweze kutoa mafunzo bora yatakayosidia vijana kufanya kazi zao kwa ufanisi wa hali ya juu pindi watakapoajiriwa au kujiajiri wenyewe.
Kuhusu maslahi kwa wafanyakazi wa Kiwanda cha A to Z, Makamu wa Rais ameutaka uongozi wa kiwanda hicho kulinda na kutetea haki za wafanyakazi kwa kutoa maslahi mazuri ambayo yatawezesha wafanyakazi hao kufanya kazi kwa bidii.
Makamu wa Rais pia amesisitiza usawa katika ulipaji wa mishahara kwa wafanyakazi wa ndani na wa nje ya nchi walioajiriwa kwenye kiwanda hicho ili kuondoa tofauti za mishahara hali ambayo ijenga motisha kwa wafanyakazi.
Kiwanda cha A to Z kilichopo eneo la Kisongo mkoani Arusha kimeajiri zaidi ya wafanyakazi 7500 ambapo asilimia 80 ya wafanyakazi wote ni wanawake.
Amewahimiza wawekezaji kote nchini walipe kodi za serikali mapema kodi ambazo zitatumika kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.