Jumatatu , 12th Jan , 2015

Serikali inatarajia kuanzisha viwanda mama mkoani Njombe kufuatia kuwapo kwa migodi ya makaa ya mawe na chuma kwa lengo la kukuza uchumi hapa nchini.

Waziri wa Biashara na Viwanda Dkt. Abdallah Kigoda.

Akizungumza kabla ya kufanya ziara katika eneo lenye machimbo ya Chuma na makaa ya mawe, Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdallah Kigoda amesema kuwa serikali ikifikilia kuanzisha viwanda itaanzisha viwanda hivyo mkoani Njombe.

Amesema kuwa viwanda mama ndio vilivyo weza kukuza uchumi wa nchi mbalimbali za ughaibuni, na kuwa hakuna nchi yoyote itakayoweza kuendelea pasipo kuwa na viwanda.

Aidha alisema kuwa katika machimbo hayo kunatarajiwa kuwapo kwa wageni kutoka china 6,000 watakao ingia katika machimbo hayo, na kuajili watanzania zaidi ya 30,000.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Njombe Dr. Rehema Nchimbi amesema kuwa Mkoa huo unatarajiwa kuwa lango kuu la uchumi wa Tanzania na kuwa siasa katika suala hili haipaswi kuingizwa.