Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Charles Mwijage
Waziri Mwijage ametoa kauli hiyo jijini Arusha, wakati wa kuadhimisha siku ya viwango duniani pamoja na kufungua mkutano mkuu wa 22 unaozungumzia nafasi ya mama na viwango na baraza la 54 la mashirika ya viwango katika bara la Afrika.
Waziri huyo wa Viwanda na biashara amesema kuwa suala la bidhaa bandia halitakua na nafasi tena na ukikutwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa huku akiongeza kuwa lengo ni kuweza kushindana na soko la kimataifa.
Aidha Waziri huyo amesisitiza kuwa serikali itakifufua kiwanda cha Kutengeneza matairi cha General Tyre, kilichopo jijini Arusha, kwa Soko la bidhaa hiyo linapatikana.