Jumanne , 6th Mei , 2014

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amesema serikali inaendelea kuboresha sekta ya sheria kwa kutoa kipaumbele katika ujenzi wa miundombinu na kuongeza idadi ya watendaji wakiwemo majaji wanawake .

Rais wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.

Mh Rais Dk. Jakaya Kikwete ameyasema hayo jijini Arusha wakati anafungua mkutano wa kimataifa wa chama cha majaji wanawake kutoka nchi mbali mbali duniani.

Aidha Rais Kikwete pia amewapongeza watendaji wanawake wa sekta ya sheria wakiwemo majaji kwa kuonyesha ufanisi mkubwa kwenye majukumu yao na kwamba mchakato wa kuongeza idadi ya wanaweke katika sekta hiyo unaendelea.

Akizungumza katika hafla hiyo jaji mkuu wa Tanzania Mh. Chande Othmani pamoja na kuelezea hatua iliyofikiwa katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta hiyo, likiwemo la uhaba wa watumishi, amesema wanaendelea kuongeza idadi ya wanawake kulingana na sifa na uwezo walionao.