Jumanne , 2nd Feb , 2016

Serikali imesema kuwa itaendelea kufanya sekta ya Utalii kuwa chanzo kikubwa cha kuliingiza pato taifa, hivyo imejipanga kuboresha miundombinu na rasilimali watu katika kuiimarisha zaidi sekta hiyo.

Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kulia) na Naibu Waziri wake Mhe. Eng. Ramo Makani (wa pili kushoto),

Akiongea leo bungeni katika kipindi cha maswali na majibu naibu waziri wa maliasili na utalii Eng. Ramo Makani amesema serikali kwa kutumia ufadhili wa dola milioni 100 inaboresha miundombinu ya viwanja vya ndege, barabara na miundombinu mingine.

Mhe. Makani amesema serikali imejipanga kutafuta miradi mingine zaidi ili kuboresha maeneo yote ambayo yatachangia katika uboreshaji wa sekta hiyo ya utalii katika kuchangua pato la taifa.

Aidha naibu waziri huyo amesema kuwa serikali pia licha ya kupanga hoteli katika madaraja pia itawasaidia wawekezaji kwa kuwasimamia ili nao waweze kufikia kujenga hoteli zenye hadhi ya kimataifa.