Jumamosi , 17th Aug , 2019

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Hamis Kigwangala amesema Serikali itaanza kuuza asilimia 10 ya mambo nje ya nchi kwa kile alichokieleza kumekuwa na ongezeko kubwa sana, wanyama wakali kuingia kwenye makazi ya watu.

Waziri amesema Serikali imejhitahidi vya kutosha kuhakikisha suala la ujangiri linaisha na nchini na wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa bali changamoto iliyopo, ni wanyama hao kuingia kwenye makazi ya watu.

"Uhifadhi na ulinzi wa maliasili nchini umeimarika na tumepata mafanikio makubwa sana. Ujangili tumeudhibiti kwa mafanikio makubwa sana"

"Changamoto mpya imezaliwa, wanyama wakali na waharibifu wamezidi na wanavamia maeneo ya watu, tumeamua kuuza asilimia 10 ya mamba wote nchini!" amesema Waziri Kigwangala

Aidha Waziri Kigwangala amesema pia Serikali itauza viboko wote waliopo kwenye maeneo yenye maji kama maziwa, mabwawa na mito iliyopo mjini, kama vile pale Mpanda, Mafia na Babati, mauzo ya wanyama yatafanyika kwa njia ya mnada kwa utaratibu ambao utatangazwa wiki ijayo.