Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage.
Akizungumza leo Bunge katika kipindi cha Maswali na majibu ambapo aliulizwa kuhisiana na uboreshaji wa viwanda Waziri Mwijage amesema mpaka sasa kiwanda hicho kinapandisha uzalishaji wake wa sukari kutoka tani 20,000 kuelekea 120,000.
Aidha, katika uwekezaji wa kiwanda cha maziwa tayari anaongea na wawekazaji ambao wameahidi kuwekeza fedha takribani shilingi bilioni 14, ambao watatengeneza mtandao wa kukusanya maziwa kuanzia mkoa wa Geita mpaka Kagera na kujenga kiwanda eneo la Misenyi.
Aidha, Waziri Mwijage ameongeza kuwa kwa sasa atahakikisha kuwa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo Vidogo (Sido), linaenea nchi nzima ili kutoa fursa ya wajasiriamali wenye viwanda vidogo kupata elimu ya kukuza biashara zao.