Ijumaa , 29th Jul , 2016

Jumuiya ya wafanyabiashara wa mafuta nchini Tanzania wameishauri serikali iweke mpango maalumu ambao utakua endelefu kwa kuboresha njia za uingizaji wa bidhaa hiyo Ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa bidhaa ya mafuta nchini .

Hayo ameyasema mwenyekiti wa Jamuhiya ya wafanyabiashara wa mafuta nchini TAPSOA bwana Farough Baghozah kwenye mahojiano maalumu nakuongeza kuwa kama serikali itaweka mpango huo itasaidia sana katika kuongeza soko la bidhaa hiyo nakupunguza ukame wa mafuta nchini.

Wameiomba serikali ielewe kuna asilimia kubwa ya wafanyabiashara wa mafuta sio waingizaji wa mafuta na kama itatokea upungufu wa mafuta basi inaweza sababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa bidhaa hizo.