Ijumaa , 3rd Jun , 2016

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Maendeleo ya Petroli(TPDC), Dkt. James Mataragio, amemuomba waziri wa nishati na Madini, kuunda tume itakayoshughulikia mikataba ya uwekezaji wa gesi asilia iliyogundulika hapa nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Maendeleo ya Petroli(TPDC), Dkt. James Mataragio

Dkt. Mataragio amesema hayo mara baada ya mazungumzo na wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, yenye lengo la kubaini changamoto zilizopo katika uwekezaji wa nishati hiyo ili zipatiwe ufumbuzi.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa kuna changomoto mbalimbali katika mikataba ya kisheria., kibiashara ambayo yanahitaji kutafutiwa ufumbuzi ili uwekezaji huo ulete tija kwa taifa na wananchi kwa Ujumla.

Dkt. Mataragio amesema tayari Wazari wa wizara hiyo ameshaut=nda timu ambayo watakutana na wawekezaji hao ili kuweza kupanga jinsi ya kufanya uendeshaji wa miradi hiyo ya gesi.

Sauti ya Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Maendeleo ya Petroli(TPDC), Dkt. James Mataragio