
Mrinde Mnzava ametoa wito huo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha East Africa Drive kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kuwa iwapo serikali itahusisha mpaka shule binafsi itawaathiri kwani kuna shule nyingine zitashindwa kujiendesha.
“Serikali ilitolee ufafanuzi tangazo hilo la Mheshimiwa Rais, na namna gani jamii imelipokea, kwa sababu jamii inaweza ikapokea kuona kwamba shule zote ni bure, lakini kumbe kuna shule za serikali na shule zisizo za serikali, tumeiomba serikali tukae meza moja, nini hatma ya shule ambazo zitashindwa kuhimili soko hilo, kwa sababu ziko shule ambazo zitashindwa kuendelea kwa sababu ya tangazo hilo”, alisema Mnzava.
Pia Mnzava amesema pamoja na tangazo hilo kutolewa bado kuna changamoto zitakazokabili utekelezaji wa agizo hilo, hivyo serikali ina wajibu wa kuliangalia kwa umakini.
“Katika hiyo elimu bure bado kuna changamoto kubwa, kwamba tangazo limetoka lakini je? miundombinu ya serikali inaruhusu kupokea zoezi hilo katika muktadha huo, kuna watoto watakaoanza Januari, kuna watoto ambao tayari wako mashuleni, je? Serikali inapotangaza elimu bure, ni kuanzia hawa wanaoanza sasa au pamoja na walioko shuleni?”, alihoji bwana Mnzava kwenye mazungumzo yake na East Africa Radio.