Ijumaa , 12th Dec , 2014

Wananchi mkoani Arusha wameombwa kujiepusha na vitendo vyovyote vinavyoweza kuvuruga Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwani serikali haitamvumilia mtu ama kikundi cha watu kitakachojaribu kuvuruga ama kutihishia amani wakati w

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. David Felix Ntibenda

Tahadhari hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. David Felix Ntebenda Kijiko alipokuwa anazungumza na viongozi na watendaji wakati anapokelewa na kukabidhiwa ofisi na amewaomba wananchi wa Arusha kuacha kutumia nguvu na rasilimali zao kuvuruga amani badala yake washirikiane na serikali kukabiliana na mamtizo yaliyopo .

Amesema zipo taarifa za kuwepo kwa baadhi watu wanaojiandaa kuvuruga uchaguzi jambo alilodai kuwa halitapata nafasi na kusisitiza wananchi kujiepusha na mtu ama kikundi chochote cha watu kinachojaribu kueneza ama kupanga njama hizo ..

Akizungumza katika hafla hiyo Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Bw, Adostine Mapunda amesema kwa upande wa watumishi na watendaji wa halmashauri wamejipanga vizuri kuhakikihsa wanatoa ushirikiano wa kutosha kuwatumikia wananchi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa zoezi la ujenzi wa maabara linakamilika.