Jumapili , 6th Jan , 2019

Serikali imeeleza kwamba imedhamiria kuwachuja Polisi Jamii ili kudhibiti uvujaji wa taarifa za kudhibiti uhalifu.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni ambapo ameeleza kwamba uratibu wa ulinzi shirikishi unahitaji kuwekewa mipango mkakati.

''Popote palipo na ulinzi shirikishi lazima uratibu wa vikundi uwe ni  jambo la msingi. Lazima watu ambao wamejitolea wachujwe, wachunguzwe na wafahamike, kwa maana tabia zao, matendo yao pamoja na hulka za" Masauni.

Masauni amesema haiwezekani, mtu anayetaka kushirikiana na jeshi la polisi bado akawa na urafiki na wahalifu.