Jumanne , 28th Jun , 2016

Waziri wa Kilimo, Maliasili , Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohammed, amesema uwekwaji wa sera na mikakati ya pamoja katika sekta ya uvuvi kwa nchi za Afrika kutaweza kusaidia upatikanaji wa soko la uhakika la kimataifa.

Waziri wa Kilimo, Maliasili , Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohammed.

Akifungua Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa kujadili masuala ya Uvuvi, pamoja na namna ya kukabiliana na masoko makuu kwa biashara za samaki Waziri Hamad amesema biashara ya samaki kwa muda mrefu imekua ikikosa soko la kimataifa kutokana na wavuvi kujishughulisha na uvuvi wa samaki wadogo.

Waziri huyo amesema kupitia Mkutano huo wataweza kujifunza kutoka kwa mataifa nje ya Afrika yaliyopiga hatua katika biashara ya samaki ili kuweza kupanua soko la bidhaa hiyo kwa nchi za Afrika.

Kwa upande wake wadau wa Mkutano huo wa Kimataifa kutoka nchini Tanzania wamesema mkutano huo utawasadia kupata ujuzi wa namna ya kutafuta soko la samaki la kimataifa ili kujikwamua kimaisha.

Mkutano huo wa Kimaitaifa umezikutanisha nchi 21 kutokaka mataifa mbalimbali duniani na kati ya hizo nchi 18 ni kutoka Afrika na Tanzania ikiwa mwenyeji wa mkutano huo.

Sauti ya Waziri wa Kilimo, Maliasili , Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar, Mhe Hamad Rashid Mohammed,