Jumanne , 26th Mei , 2015

Sekta ya Biashara nchini Tanzania imekuwa kwa asilimia 10 kwa mwaka 2014 ukilinganisha na asilimia 4.5 mwaka 2013 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 5.5

Waziri wa viwanda na Biashara Dkt. Abdallah Kigoda.

Akisoma Bajeti ya Wizara ya viwanda na Biashara leo Bungeni Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdallah Kigoda amesema ongezeko hilo limetokana na bidhaa za kilimo na viwandani pamoja na bidhaa kutoka nje.

Dkt. Kigoda ameongeza kuwa kulingana na takwimu ya sekretariteti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki mauzo ya Tanzania katika soko la jumuiya yameongezeka toka dola milioni 158 mwaka 2013 hadi kufikia dola 723 kwa m waka 2014.

Aidha Dkt. Kigoda amesema Serikali imekubaliana na wadau mbalimbali kwa ajili ya kununua hisa za asilimia 26 katika kiwanda kcha kutengenza matairi jijini Arusha ambapo itafanya serika imiliki kiwanda hicho kwa asilimia 100.

Amesema lengo la kufufuliwa kwa kiwanda hicho ni kufufua mashamba ya mipira pamoja na kutoa fursa za ajira nchini.

Mh. Kigoda amesema kuwa mradi huo utafufua mashamba ya Kihuhu Muheza na kalunga kilombero na tayari miti laki mbili na arobaini imekwisha patikana pia itatoa fursa za ajira zaidi ya 1050.