Jumatano , 4th Mar , 2015

Serikali imeitaka sekta binafsi nchini kuwekeza katika Nishati mbadala ili kuisaidia serikali kufikia malengo ya kuwalete wananchi maendeleo.

Kamishna Msaidizi wa Nishati Mbadala kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Leonard Ishengoma.

Hayo yamesemwa na Kaimu Kamishna wa Nishati Mbadala toka Wizara ya Nishati na Madini Mwandisi, Paulo Kiwele wakati akimwakilisha katibu Mkuu katika Uzinduzi wa Nishati ya Umeme jua ya hali ya juu.

Kiwele ameongeza kuwa Nishati ya Umeme wa jua ni Nishati mbadala na itasaidia sana katika uchumi wa nchi hasa maeneo ya vijijini ambapo itawasaidia watu wenye Vipato vidogo kuanzisha viwanda vidogo ili kujikwamua kiuchumi.

Kwa Upande wake mdau wa Umeme jua amesema wanataka kuwafikia Watanzania zaidi ya million moja maeneo ya vijijini ili kuisaidia serikali kufikia malengo yake ya kuwa nchi yenye viwanda na kipato cha kati mwaka 2025