
Nembo ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC.
Katika Mkutano huo uliofanyika kwa njia ya mtandao Tanzania imewakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula aliyeambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Joseph Edward Sokoine ambapo takwimu zinaonesha kupungua kwa maambukizi na vifo katika bara hilo.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa katika kipindi cha Januari hadi Mei 2021 Bara la Afrika limeripotiwa kuwa na visa vipya arobaini na mbili elfu ambapo vifo vipya ni zaidi ya elfu moja na hivyo kushauri kuwa mikutano ya Jumuiya hiyo katika ngazi mbalimbali iendelee kufanyika kwa mseto wa ana kwa ana au kwa njia ya mtandao.
Katika tukio jingine Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amefanya mkutano kwa njia ya mtandao na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Mhe. Ine Eriksen ambaye ameeleza kuridhishwa na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya sita katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji pamoja na masuala ya utawala bora na haki za binadamu.