
Mama Samia Suluhu Hassan, mgombea mwenza wa rais kupitia CCM
Samia amesisitiza juu ya kauli ambayo imekuwa ikitumiwa na mgombea Urais kupitia chama chake Dkt. John Magufuli kuwa maendeleo hayana chama na kuwataka wananchi wa eneo hilo bila kujali vyama vyao wawachague wagombea wa CCM ili luendeleza safari ya maendeleo ambayo imekuwa ikisimamiwa na chama hicho.
''Sasa ndugu zangu hamna haja ya kupoteza nguvu zenu kipiga kura upande mwingine wowote ule, ni sawa na kwamba unachukua fedha yako unatia shimoni haina faida haina tija niwaombe wana Mkarama wote wa vyama vyote kura yako ndiyo maendeleo yako, piga kura kwa Chama cha Mapinduzi ili twende na safari yetu ya maendeleo” amesema . Mama Samia.
Aidha Suluhu amewataka wapiga kura hao kuwa makini na wagombea wa vyama vingine ambao wanakuja na kuomba ridhaa ya kuwaongoza kwa kipindi cha miaka mitano ijayo, ambapo amekitaja chama chake kuwa ndicho kinastahili kupewa dhamana hiyo kwa sasa.
''Watakuja wengine hapa labda wabunge, waje wasimame wakuambieni nitafanya nitafanya swali la kuuliza ni moja tu atafanya kwa serikali gani, kwa sababu serikali bado itabaki ya Chama cha Mapinduzi, yeye atakaye kuja kufanya atafanya kwa serikali gani na kama ni mipango lazima afuate Ilani yetu ya Chama cha Mapinduzi'', amesema Mama Samia