Pweza wakiwa wamechemshwa
Akizungumza na East Africa Radio katika kipindi cha East Africa Break Fast Prof. Kaale amesema taarifa za utafiti wa wanafunzi wa Muhimbili bado haujakamilika kwani umeishia katika hatua ya wanyama panya na majaribio kabla hayajaenda kwa binadamu lazima yafanyike kwa wanyama wenye mfumo unaofanana kwa kiasi fulani na binadamu.
"Mwanafunzi alinunua pweza akamchemsha mwenyewe, akawapa panya mchuzi akawafuatilia kwa muda wa siku 29 na aliwatenga panya katika makundi mawili kundi moja likapewa maji na lingine likapewa mchuzi wa pweza na mfumo wa ‘genetics’ unafanana sana na binadamu kwa zaidi ya asilimia 95 lakini hatuwezi kusema kwamba umethibitishwa kwa binadamu bila hatua zote kukamilika" Amesema Prof. Kaale
Prof. ameendelea kufafanua kwamba waliopewa supu walionekana kufanya tendo la kujamiiana mara nyingi kuliko wale waliopewa maji hivyo kisayansi huwezi kusema moja kwa moja kwamba tayari na kwa binadamu supu hiyo inaweza kufanya kazi.
Aidha Prof. Kaale ambaye ndiye alisimamia utafiti huo wa awali, amesema hatua zaidi juu ya utafiti huo zitaendele ili kuangalia tena wanyama wengine kabla ya majaribio ya kuja kujiridhisha kwa binadamu.