Air Tanzania
Waziri Dkt. Chana amesema uwepo wa safari za ndege za Tanzania za moja kwa moja hadi Dallas nchini Marekani zitasaidia kuongeza idadi ya wageni wataokuja nchini kutembelea hifadhi na ameneo yote ya utalii, haya yakiwa ni matokeo chanya ya filamu ya Royal Tour.
Aidha hapo jana wakati wa mawasilisho ya makadirio ya bajeti ya Wizara ya Maliasili bungeni Dodoma, baadhi ya wabunge waliishauri serikali kuongeza kasi ya kutatua changamoto ya migongano kati ya binadamu na wanyamapori ambayo inahusisha Hifadhi na makazi ya wananchi.


