Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Saba toka upinzani wajiunga CCM rasmi leo

Ijumaa , 25th Mei , 2018

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepokea wanachama saba kutoka vyama vitatu vya upinzani ambao wameamua kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM) na wengine 82 kutoka Chama cha Wananchi (CUF) ambao walikuwa wapiga debe.

Wanachama hao wamepokelewa leo mchana Mei 25, 2018 wakati akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua uwanja mpya wa michezo unaojengwa katika kijiji cha Dodoma, kata ya Nachingwea, wilayani Ruangwa, mkoani Lindi.

Waziri Mkuu ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, alipokea kadi nne za CUF, moja ya ACT na mbili za CHADEMA kutoka kwa wanachama hao saba kabla hajawakabidhi kadi za CCM. Wanachama hao saba waliokabidhiwa kadi mpya za CCM pamoja na wenzao 82, walikula kiapo cha uaminifu mbele ya Waziri Mkuu.

Shangwe zililipuka uwanjani hapo wakati aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CHADEMA kata ya Nachingwea, Bw. Ismail Hamisi alipokabidhi kadi yake kwa Waziri Mkuu.

Akisoma risala kwa niaba ya wanachama wenzake walioamua kujiunga na CCM, mkazi wa Ruangwa mjini, Bw. Fred Mnimbo amesema wameamua kurudi kwa sababu yale waliyotarajia yafanyike upinzani hayaonekani.

“Tumegundua upinzani wa sasa ni maslahi binafsi na si wa kuwatumikia wananchi, kinachosemwa sicho kinachotendwa na wapinzani na pia tumeamua kuunga mkono juhudi anazofanya Rais John Pombe Magufuli,”amesema Bw. Mnimbo

Mnimbo amesema wameamua kuhamia CCM kwa sababu serikali iliyopo madarakani kwa sasa inatekeleza mahitaji ya watanzania kwa asilimia 90 na pia wanataka kumuunga mkono mbunge wao wakiwa katika chombo kimoja ili waijenge vizuri Ruangwa na Tanzania kwa ujumla.

Novemba 5, mwaka jana, Waziri Mkuu alipokea wanachama 37 kutoka vyama vya CUF na CHADEMA kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Mbekenyera, wilayani Ruangwa. Pia Desemba 29, 2017, alipokea wanachama 60 kutoka CUF kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Nkowe kata ya Nkowe, wilayani Ruangwa.

HABARI ZAIDI

Sehemu ya Ardhi iliyoathirika na Mabadiliko ya Tabia Nchi

Hizi hapa sababu za hali ya hewa isiyotarajiwa

Picha za Satelaiti Zikionyesha Mwenendo wa Kimbunga Hidaya

Kimbunga Hidaya chaendelea kutawala eneo la Pwani

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wanahabari na Wadau wengine kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo Mei 03, 2024.

Watendaji serikalini ondoeni ukiritimba - Majaliwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi