Akizungumza leo Jijini Dar es salaam katika mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa),Mkurugenzi wa Asasi ya Agape Aids Control John Miola anasema vyombo vya maamuzi vimekuwa vikichangia kuongezeka kwa ndoa za utotoni mkoani Shinyanga
John Miola anasema hali hiyo imewaathiri watoto wengi mbali ya kuwa mila na desturi, Migogoro ya kifamilia inapelekea wazazi kutengana huku suala la Daktari kutotoa ushiriakiano kwa binti aliyebakwa katika kijiji cha Shagihilu hapo Disemba 25,mwaka jana likionekana kumuathiri zaidi.
Mkoa wa Shinyanga unaongoza kwa kuwa na asilimia 59 ya ndoa za utotoni ukifuatiwa na Tabora asilimia 58 na watatu ukiwa ni moa wa Mara wenye asilimia 55 huku aliyekuwa mkurugenzi wa Tamwa Valerie Msoka akisema tatizo la mimba na ndoa za utotoni ni kubwa barani Afrika.
