Jumatatu , 16th Sep , 2019

Staa wa filamu Rose Ndauka amenyoosha maelezo kuhusu kumiliki kibenten, mwanaume anayemtaka, kuumizwa kwenye mapenzi na issue za baba wa mtoto wake.

Rose Ndauka akiwa na mwanaume.

'Issue' ya kibenten Rose Ndauka ameileza EATV & EA Radio Digital, baada ya kupost picha katika mtandao wa Instagram na kuandika kuwa yupo na kibenten.

"Unajua Instagram kuna watu vitu wanapenda na niliandika vile nilijua watu watatiririka tu, lakini sio kweli yule ni mdogo wangu tu, niliandika kuwa nipo na 'kiben.... whaaat' ila watu wamejieleza lakini sikuwa nimeweka wazi ila nilijua akili ya watanzania watasema nini".

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Mimi tena na kiben.......what  Weweeeee.....Ahsante kwa zawadi,Mnisaidie kumtag ❤️

A post shared by Rose Donatus Ndauka (@rossendauka) on

Aidha Rose Ndauka ameendelea kusema hawezi kuwa na mahusiano na kibenten na hajaona sababu ya kuwa na kibenten ila alishawahi kuumizwa kwenye mapenzi na alichukulia kama funzo.

Pia amesema anapenda kuwa na mwanaume mchapakazi anayependa familia aliyekamilika na hamtaki mwanaume anayelala kitandani tu.

Kuhusu 'issue' za kumficha baba wa mtoto wake Rose Ndauka amesema sio mbaya kama yeye pekee akimjua mtoto wake na baba wa mtoto inatosha licha ya watu kusema amemtengana na mzazi mwenziye na hatoi malezi kwa watoto ndiyo maana hamuonyeshi.