Mkurugenzi wa masuala ya utafiti wa REPOA Bw. Donald Mmari amesema hayo leo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya mkutano wa 19 utakaozungumzia mabadiliko, ajira na kutokomeza umasikini unaotarajiwa kufanyika Jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 9 na 10 mwezi huu na kufunguliwa na Rais Jakaya Kikwete.
Amesema katika kipindi cha miaka kumi iliyopita uchumi wa nchi umekuwa ukikua kwa wastani wa asilimia 6 hadi 7 kwa mwaka, lakini pamoja na kukua kwa uchumi huo bado hali ya umasikini kwa mtanzania ni kubwa hivyo kupitia mkutano huo wataweza kujadili namna ya kuboresha tafiti hizo ili ziweze kumsaidia mtanzania wa kawaida.