
Baadhi ya waalimu wa mkoa wa Dar es Salaam waliohudhuria kikao kazi kilichoitishwa na Mkuu wa mkoa huo.
Rai hiyo ameitoa katika kikao kazi kilichowakutanisha baadhi ya walimu kutoka katika kata mbali mbali za manispaa ya Ilala pamoja na watumishi kutoka ngazi ya manispaa pamoja na kutambua changamoto na jitihada kubwa zilizofanywa na waalimu katika ngazi ya shule za msingi.
"Nitumie fursa hii kuwapa onyo walimu hasa shule za sekondari wanaoungana na wamiliki wa shule kuiba mitihani ama kufanya udanganyifu wowote hiyo tabia iache Mara Moja haitavumilika"alisema Abubakar Kunenge
Awali akitoa taarifa ya hali ya ukusanyaji wa mapato ulivyo kwa sasa mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri amesema zaidi ya bilioni 58 zimekusanywa huku manispaa hiyo ikizidi kupata hati safi kwa miaka minne mfululizo.
Kwa upande wa walimu waliohudhuria katika mkutano huo wamesema vikao kazi ndo msingi wa ufanisi kwakuwa hukumbusha majukumu kiutendaji ikiwa ni pamoja na kuwasilisha changamoto wanazokumbana nao ili ziweze kupatiwa ufumbuzi.