Mhe. Rais Magufuli akiweka jiwe la msingi leo katika ufunguzi wa barabara ya Kigoma-Biharamulo-Lusahunga yenye urefu wa Kilometa 154.
Rais Magufuli ametoa agizo hilo wakati wa ufunguzi wa barabara ya Kigoma-Biharamulo-Lusahunga yenye urefu wa KM 154 huku akiwataka mawaziri wenye dhamana kuhakikisha wanafuatilia maagizo hayo kuanzia sasa.
"Wanaolalamika kukosa mafuta waendelee kufanya hivyo, ni mara mia tukose mafuta kuliko kuwa na wafanyabiashara wanaokwepa kodi", amesema Rais Magufuli.
Pamoja na hayo, Rais Magufuli amewataka wafugaji waliovamia hifadhi ya Burigi Mkoani Kagera kuondoa mifugo yao mara moja na amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu kuendelea na operesheni ya kuondoa mifugo yote iliyovamia hifadhi hiyo na maeneo mengine yasiyoruhusiwa kupeleka mifugo.
“Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya simamieni hilo, ninajua bado kuna ng’ombe mle hifadhini, simamieni kwa kuzingatia sheria za hifadhi. Kwa hiyo wafugaji wajifunze namna ya kufuga, kama unaona una ng’ombe wengi na huwezi kuwatunza uza, hata mimi nimeuza ng’ombe wangu niliona wamekuwa wengi siwezi kuwatunza, viwanda vipo” amesisitiza Rais Magufuli.
Kwa upande mwingine, Rais Magufuli amepiga marufuku wananchi kutozwa kodi kwa mzigo wenye uzito wa tani moja anapousafirisha kutoka wilaya moja kwenda nyingine.



