Jumatano , 16th Nov , 2016

Rais wa Syria Bashar Al Assad amesema kuwa Rais mteule wa Marekani Donald Trump anaweza kuwa mshirika wake iwapo atafuata ahadi zake za kukabiliana na magaidi.

Bashar Al Assad (Kushoto) , Donald Trump (Kulia)

 

Kauli za Al Assad zilitangazwa saa chache baada ya Urusi kuanz upya mashambulio yake nchini Syria mashambulio  yanayolenga kundi la Islamic State pamoja na waasi wenye uhusiano na Al-qaeda.

Assad amesema atatakiwa kusubiri kuona kama Trump ataweza kuleta mabadiliko katika sera ya Marekani dhidi ya Syria.

Wakati wa kampeni zake Trump aliahidi kuwamaliza wapiganaji wa jihad wa Islamic State.