Rais Samia kuhutubia bunge Aprili 22, 2021

Jumatatu , 19th Apr , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan Aprili 22, 2021, atalihutubia bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan

Hotuba yake hiyo inatarajiwa kueleza malengo na mwelekeo mzima wa serikali yake ya awamu ya sita. 

Hotuba hiyo inatarajiwa kuanza saa 10:00 jioni, bungeni jijini Dodoma.