Jumapili , 27th Mar , 2022

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amesema kama kuna mtu ana ndoto au anaota kwamba Rais Samia Suluhu Hassan atashindwa kuliongoza taifa, basi ndoto hiyo haiwezi kutimia.

Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi

Shaka Hamdu Shaka, ameyasema hayo katika  kongamano la kumpongeza Rais Samia kutokana na uongozi wake wenye kugusa maendeleo ya wananchi katika kipindi cha mwaka mmoja, kongamano hilo limefanyika Jijini Mwanza.

''Waliodhania hawezi, mama shupavu amesimama imara. Na mimi nataka niwambie kama kuna mtu ana ndoto au anaota kwamba Rais Samia atashindwa kuliongoza Taifa hili, huyo mtun asahau kwasababu Rais Samia anakwenda kufanya maajabu makubwa sana'' - Shaka Hamdu Shaka.

Aidha, Shaka amesema Rais Samia amejipambanua katika kuendeleza mema yaliyoanzishwa na watungulizi wake kuanzia awamu ya kwanza na kwamba kuna uhakika wa kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya 2020-2025 kwa zaidi ya asilimia 99.

Akitoa mada katika kongamano hilo, Mhadhiri wa Chuo Kikuucha Mtakatifu Joseph Tanzania (SAUT), Kampasi ya Mwanza amesema katika kipindi cha mwaka mmoja Rais Samia ameonyesha uwezo wa kutafuta fursa zote za ndani na nje ya nchi kwa maslahi ya taifa.