Jumatatu , 2nd Oct , 2023

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua George Mandepo kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania ambapo kabla ya uteuzi alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Usuluhishi, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali na amechukua nafasi ya Griffin Venance Mwakapeje

Rais Samia Suluhu Hassan

Ambaye aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Rais Samia amemteua Saudin Jacob Mwakaje, kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Sanaa la Taifa. Dkt Mwakaje ni Mhadhiri mwandamizi chuo kikuu cha Dar es Salaam na mjumbe wa baraza lililomaliza muda wake

Aidha Rais Samia amemteua George Daniel Yembesi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la chuo kikuu cha ushirika Moshi (MoCU) kwa kipindi cha pili