Jumanne , 6th Feb , 2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan, amemteua Abdul-Razaq Badru kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), kabla ya uteuzi huo alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).

Kushoto ni Abdul-Razaq Badru aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na kulia ni Dkt Bill Kiwia aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa hii leo februari 6, 2024, ambapo pia amemteua Dkt Bill Kiwia kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).

Aidha Rais Samia amemteua Dkt Thomas Nestory Bwana kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), na kabla ya uteuzi huo alikuwa ni Mkurugenzi Msaidizi Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais na anachukua nafasi ya Dkt. Geofrey Mkamilo ambaye amemaliza muda wake