
Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mwanahamisi Athumani Munkunda na kumteua Mobhare Holmes Matinyi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke.
Aidha ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Abel Yeji Busalama. Amemhamisha kituo Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mjini, Hashim Shaib Mgandilwa kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilindi.
Pamoja na hayo Rais Samia amemteua James Wilbert Kaji kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mjini