Jumatatu , 15th Jul , 2024

Wizara ya Kilimo imempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuonesha nia ya dhati katika kukuza sekta ya kilimo hivyo wakulima watumie fursa hiyo kufanya kilimo cha kisasa na wadau mbalimbali wawekeze katika kilimo kwa kuwa kina fursa nyingi zinazoweza kuinua pato la Taifa na mwananchi.

Rais Samia Suluhu Hassan

Hayo yamebainishwa Mohamed Chikawe ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango na Bajeti katika Idara ya Sera na Mipango Wizara ya Kilimo na kusema maonesho ya kimataifa ya kilimo maarufu kama Nanenane kwa mwaka huu yatasaidia kukuza mahusiano ya kibiashara na kutanua wigo wa soko la mazao ya kilimo na bidhaa za kilimo ndani na nje ya mipaka ya Tanzania  kutokana na  ushiriki wa wadau mbalimbali wa kisekta.

"Maonesho ya kimataifa ya Nanenane yatafungua fursa za masoko ya bidhaa zetu na kuongeza ushirikiano wa kimataifa na nchi mbalimbali katika Sekta ya kilimo, jambo litakalosaidia kutanua wigo wa kimasoko na kutatua changamoto mbalimbali kwenye kilimo hususan katika mabadiliko ya tabianchi, upatikanaji wa mbegu bora na kufanya utafiti ili kuweza kutatua changamoto hizo pamoja na kusaidiana katika uzalishaji," amesema