Jumanne , 23rd Mei , 2023

Rais Samia Suluhu Hassan, amemteua Kenani Kihongosi kuwa Mkuu wa wilaya ya Urambo, akichukua nafasi ya Mohamed Mtanda ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa mkoa wa Mara.

Kushoto ni Mkuu mpya wa mkoa wa mara Said Mohamed Mtanda na kulia ni Kenani Kihongosi ambaye ni DC mpya wa Urambo

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo Mei 23, 2023, ambapo Rais Samia amemteua Said Mohamed Mtanda kuwa Mkuu wa mkoa wa Mara, akichukua nafasi ya Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee, ambaye atapangiwa majukumu mengine.

Mbali na kuteua Rais Samia amemhamisha Charles Makongoro Nyerere kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, ambapo awali alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara na amechukua nafasi ya Queen Sendiga ambaye amehamishiwa Manyara.