Alhamisi , 11th Jul , 2024

Rais wa Kenya William Ruto amevunja Baraza lake la Mawaziri hii leo Julai 11, 2024 pamoja na kumuondosha madarakani Mwanasheria Mkuu wa serikali na agizo hilo linaanza kutekelezwa mara moja.

Rais wa Kenya William Ruto

Makamu wa Rais Rigathi Gachagua na Waziri Mkuu wa Baraza la Mawaziri Musalia Mudavadi pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje ya Kenya watabaki na vyeo vyao.

Kenya imekumbwa na maandamano ya kupinga hali ngumu ya maisha yaliyosababisha vifo na majeruhi kwenye miji kadhaa ukiwemo mji mkuu wa Nairobi.